VIDEO: Harmonize atoa sababu ya 'Kondeboy Mgahawa' kutoonekana mtaani

Wednesday January 15 2020

Mwanaspoti-Harmonize-Kondeboy Mgahawa-Tanzania-Mwanasport-MICHEZO-Michezo blog

 

By Nasra Abdallah

Dar es Salaam.Mwanamuziki Harmonize aeleza sababu ya mgahawa wake alioupa jina la 'Kondeboy Mgahawa' kutoonekana mtaani.

Harmonize jina lake halisi ni Rajabu Abdul, ameyasema hayo leo January 15, 2020 katika mkutano na waandishi wa habari uliohusu kutangazwa kuwa balozi wa kinywaji cha Twist.

Harmonize alizundua mgawaha huo Oktoba 20, 2019 ambao ni wa gari kwa lengo la kugawa chakula bure mtaani kila siku ya Jumapili, lakini baadaye haukuonekana.

Harmonize amesema gari hilo lilijikuta likifanya shughuli hiyo kwa Jumapili tano waliacha baada ya kampuni ya Sayona kuomba kuwaunga mkono katika hilo.

Kutokana na hatua hiyo, amesema sasa watakuwa na magari matatu badala ya moja ambayo yatakuwa yakipita mitaa mbalimbali na huenda na siku za kutoa chakula zikaongezeka.

"Tuambizane ukweli sisi wenyewe hatuwezi kuwalisha watu wote Dar nzima na kwa kuanza na gari moja ilikuwa ni katika kuonyesha nia yetu ya kuwasaidia wachache tuliojaliwa.

Advertisement

"Hivyo ujio wa Sayona katika kutuunga mkono kwenye hili sisi kwetu ni faraja kubwa na nina imani tutawafikia watu wengi," amesema Harmonize.

Advertisement