Vibonde Mbao FC wawavutia kasi Tanzania Prisons

Muktasari:

Mbao FC kwa sasa ipo nafasi ya 19 katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania ikiwa na pointi 22 baada ya kucheza mechi 28 hadi sasa.

Mwanza. Mbao FC kesho Jumanne watakipiga na Tanzania Prisons lakini

Kocha Msaidizi wa Mbao FC, Agustino Malindi amesema kwa sasa wako katika hali mbaya katika msimamo wa Ligi Kuu hivyo ni lazima washinde mchezo kesho dhidi ya Tanzania Prisons.

Mbao FC kwa sasa ipo nafasi ya 19 katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania ikiwa na pointi 22 baada ya kucheza mechi 28 hadi sasa.

Malindi alisema mambo yamekuwa magumu kwao hivyo kitakachoweza kuwaokoa ni kushinda mechi zilizobaki kuanzia na kesho dhidi ya Tanzania Prisons.

“Tuko katika hali mbaya katika ligi tunahitaji pointi tatu hivyo tumejipanga huu mchezo wetu na Tanzania prisons tuweze kupata ushindi angalau utatusaidia katika kuhakikisha tunabaki msimu ujao,”alisema Malindi.

Kocha huyo alisema hakuna kingine ambacho kitaweza kuwaokoa washishuke daraja kwa sasa zaidi ya kupata ushindi katika michezo 10 ya ligi hiyo iliyobaki.

Alisema wameshafanya marekebisho katika kikosi chao haswa upande wa ulinzi ambapo mabeki wao walikuwa hawako vizuri katika ukabaji jambo ambalo lilifanya wafungwe mabao ya kizembe.