Stamina: Sina mpango na siasa, mimi ni muziki tu

Muktasari:

Nitampigia na nyingine nyingi zikiwemo zile alizofanya na kundi la Rostam akiwa na msanii Roma Mkatoliki, amesema hataki kuingia kwenye siasa labda watu wamuingize kutaka kuongozwa.

MSANII wa muziki wa kizazi kipya,  Stamina amesema hana mpango wa kuingia kwenye siasa, licha ya kuonekana akikosoa sana wanasiasa kupitia baadhi ya nyimbo zake.
Stamina jina lake halisi Bonivanture Kabongo ametamba na nyimbo kama Kabwela, Mwambie, Najuta Kubalehe, Nitampigia na nyingine nyingi zikiwemo zile alizofanya na kundi la Rostam akiwa na msanii Roma Mkatoliki, amesema hataki kuingia kwenye siasa labda watu wamuingize kutaka kuongozwa.
"Masuala ya siasa na mimi ni vitu viwili tofauti, sijawahi kuwaza kuingia kwenye siasa ila ikatokea watu wakataka kunichagua niwaongoze, niko tayari ila siyo mimi kuwafuata kuomba kura," amesema Stamina
Stamina alisema anafurahi kufanya muziki na wala hajuti kwa kuwa unamwongezea kipato kikubwa, kitu kikubwa ni kutunga nyimbo zenye maudhui mazuri na mvuto na kwa wakati husika.