Mwanamuziki Hussen Machozi awashangaa waliomzushia kifo

Thursday March 26 2020

Mwanaspoti, Tanzania, Mwanamuziki Hussen Machozi, awashangaa waliomzushia, kifo, Corona, Italy

 

By RHOBI CHACHA

Dar es Salaam. Mwanamuziki Hussein Machozi amewashangaa watu waliomzushia kuwa amekufa kwa sababu anaishi nchini Italia.

Machozi ametuma kipande cha video katika akaunti yake ya Instagram, kinachosema Watanzania waache kumzushia kifo yeye sio mtu wa kiki za kifo kwani habari hizo hii ni mara ya pili.

Machozi kwasasa anaishi Italia amezungumza zaidi kwenye hiyo video kuwa kama kuna kitu amewakosea Watanzania wamwambie ili aombe radhi asamehewe.

Mwaka 2015 Hussein Machozi alizushiwa kifo na baadae alikanusha na akaiomba mamlaka husika iwafuatilie watu wanaotumia vibaya juu ya usambazaji wa habari hizo.

Habari hizo za uzushi wa kifo mwaka 2015, zilipelekea mama yake mzazi kuumwa presha na pia dada yake kuanguka ghafla alipokuwa kwenye shughuli zake za kutafuta riziki.

Hussein Machozi amewahi kutamba na wimbo Unanifaa, Mimi na nawe, Manyoni sio mbali, Nipe sikuachi na nyingine nyingi.

Advertisement

Advertisement