Cheki ‘birthday’ ya Ronaldinho akiwa rumande

Muktasari:

Ronaldinho kati alitimiza umri wa miaka 40, alisheherekea sikukuu yake ya kuzaliwa akiwa rumande anakoendelea kusubiri hatma yake baada ya kutuhumiwa kwa kosa la kuingia Paraguay kwa kutumia hati feki ya kusafiria.

ASUNCION, PARAGUAY, KWANI kuna mtu hajui kuwa Ronaldinho Gaucho yuko rumande? Kama yupo basi habari ndiyo hiyo. lakini, pamoja na hali hiyo staa huyo amesherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kujichana nyama za kuchoma za kutosha huko huko korokoroni.
Gwiji huyu wa Samba ambaye juzi kati alitimiza umri wa miaka 40, alisheherekea sikukuu yake ya kuzaliwa akiwa rumande anakoendelea kusubiri hatma yake baada ya kutuhumiwa kwa kosa la kuingia Paraguay kwa kutumia hati feki ya kusafiria.
Picha ya Ronaldinho akiwa na mapande ya nyama za kuchoma ilisambaa mitandaoni huku ikielezwa ilikuwa ni sehemua yake ya kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.
Mbali na kujichana nyama za kutosha, Ronaldinho alipata ujumbe kutoka kwa mastaa mbalimbali ambao walikuwa wanamtakia heri ya kuzaliwa gwiji huyo mtukutu wa Kibrazil.
Miongoni mwa mastaa waliomtakia kila la kheri Gaucho katika siku yake ya kuzaliwa alikuwa ni Ronaldo de Lima, Roberto Carlos, Pele, Samuel Eto’o  na wengine wengi huku wakiweka video na picha zake enzi akiwa uwanjani.