Mwakinyo si mtu wa mademu kabisa!

Thursday September 13 2018

 

By Burhani Yakub

Tanga. Vijana wa maskani ya Domozege iliyopo Makorora Jijini Tanga ambayo ndio iliyomtoa bondia, Hassan Mwakinyo, wamesema jamaa huyo si mtu wa starehe kabisa.

Jamaa hao wamesema, Mwakinyo amefanikiwa kwa sababu hashiriki mambo yoyote ya anasa kama unywaji wa pombe, uvutaji wa sigara na mademu.

Wamesema, Mwakinyo amekuwa mtu wa mazoezi na mwenye kuipenda kazi yake.

Juma Salehe ambaye ni jamaa wa Mwakinyo katika maskani hiyo ya Domozege amesema, bondia huyo atafanikiwa kwa sababu ya mambo hayo.

“Hassan ni kijana ambaye atafika mbali kwa sababu si mtu wa kupenda mambo ya anasa kama ilivyo kwa vijana wengine. Anafanya mazoezi na anapotoka ni kupumzika nyumbani tu, huwezi kumwona kwenye maswala ya pombe na mambo mengine yasiyofaa kama mademu na

ulevi,'alisema Salehe.

Chipukizi huyo, aliyejizolea umaarufu kwenye ndoni baada ya kumpiga kwa TKO

 Sam  Egginton wa Birmingham, England.

Advertisement