Mwakinyo: Mcongo hanitishi kwa lolote

Muktasari:

Licha ya Tshibangu kuwa na rekodi ya kutopigwa katika mapambano 12 aliyokwishacheza, Mwakinyo amesema rekodi hiyo si kitu kwake.

WAKATI homa ya kuwania ubingwa wa mabara wa WBF kati a Hassan Mwakinyo na Tshibangu Kayembe ikipanda, Mwakinyo amewatoa hofu mashabiki wake akisisitiza kuwa mpinzani wake raia wa DR Congo hamtishi kwa lolote.

Mabondia hao watazichapa Ijumaa ijayo pambano la raundi 12 la uzani wa super welter litakalopigwa kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Mpinzani wa Mwakinyo anatarajiwa kuwasili nchini wakati wowote kuanzia sasa  tayari kwa zoezi la kupima uzito na afya litakalofanyika keshokutwa Alhamisi.

Mwakinyo anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam kesho Jumatano akitokea Tanga ilipo kambi yake, ambayo anasisitiza kuwa ni kambi ya mafanikio.

"Mashabiki wangu wajiandae kupokea ubingwa, Mcongo hanitishi kwa lolote," amesema Mwakinyo.

"Ninachosubiri ni siku ya pambano ifike, mashabiki wangu wakae mkao wa kusherehekea ubingwa mapema, hata iweje Tshbangu hawezi kunipiga," amejinasibu Mwakinyo ambaye ana rekodi ya kucheza mapambano 18 na kushinda 16.

Pambano hilo litatanguliwa na mengine 10 ambapo Tony Rashid atazichapa na Yamikani Mkandawire, Haidari Mchanjo dhidi ya Baina Mazola, Issa Nampepeche na Khalid Manje, Selemani Kidunda atacheza na Shabani Kaoneka, Mussa Chitepete atamkabiri Bakari Mohamed Nhumba, Hamidu Kwata na Ali Ngwando, Juma Ramadhani Choki na Emmanuel Mwakyembe

 Said Zungu atacheza na Ismail Galiyatano, wakati wapinzani wa Stumai Muki na Ramadhani Shauri wakitajwa hivi karibuni.Licha ya Tshibangu kuwa na rekodi ya kutopigwa katika mapambano 12 aliyokwishacheza, Mwakinyo amesema rekodi hiyo si kitu kwake.

WAKATI homa ya kuwania ubingwa wa mabara wa WBF kati a Hassan Mwakinyo na Tshibangu Kayembe ikipanda, Mwakinyo amewatoa hofu mashabiki wake akisisitiza kuwa mpinzani wake raia wa DR Congo hamtishi kwa lolote.

Mabondia hao watazichapa Ijumaa ijayo pambano la raundi 12 la uzani wa super welter litakalopigwa kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Mpinzani wa Mwakinyo anatarajiwa kuwasili nchini wakati wowote kuanzia sasa  tayari kwa zoezi la kupima uzito na afya litakalofanyika keshokutwa Alhamisi.

Mwakinyo anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam kesho Jumatano akitokea Tanga ilipo kambi yake, ambayo anasisitiza kuwa ni kambi ya mafanikio.

"Mashabiki wangu wajiandae kupokea ubingwa, Mcongo hanitishi kwa lolote," amesema Mwakinyo.

"Ninachosubiri ni siku ya pambano ifike, mashabiki wangu wakae mkao wa kusherehekea ubingwa mapema, hata iweje Tshbangu hawezi kunipiga," amejinasibu Mwakinyo ambaye ana rekodi ya kucheza mapambano 18 na kushinda 16.

Pambano hilo litatanguliwa na mengine 10 ambapo Tony Rashid atazichapa na Yamikani Mkandawire, Haidari Mchanjo dhidi ya Baina Mazola, Issa Nampepeche na Khalid Manje, Selemani Kidunda atacheza na Shabani Kaoneka, Mussa Chitepete atamkabiri Bakari Mohamed Nhumba, Hamidu Kwata na Ali Ngwando, Juma Ramadhani Choki na Emmanuel Mwakyembe

 Said Zungu atacheza na Ismail Galiyatano, wakati wapinzani wa Stumai Muki na Ramadhani Shauri wakitajwa hivi karibuni.