Mwadui yashinda Kocha Bizimungu apagawa

Muktasari:

Tangu kuanza kwa Ligi Kuu msimu huu Agosti 22, Mwadui ilikuwa haijaonja ushindi wowote na kujikita mkiani mwa msimamo wa ligi.

MWANZA. Licha ya kufanikiwa kuonja ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu Bara Mwadui FC,

Kocha wa Mwadui, Ally Bizimungu amesema pamoja na kupata furaha ya kuondoa gundu kwa ushindi dhidi ya Biashara United, bado ana kazi ngumu kukiweka fiti kikosi chake.

Mwadui inaburuza mkia kwa pointi tano, ilisota katika mechi zake saba sawa na dakika 630 bila kushinda huku ikichezea sare na vichapo, ambapo jana ilitoa gundu kwa kuikandika Biashara United mabao 2-0 mchezo uliopigwa mkoani Mara.

Kocha Bizimungu alisema alisema ushindi huo wa kwanza katika Ligi Kuu, lakini bado ana kazi ya ziada ya kukiandaa zaidi kikosi chake ili mechi zinazofuata waweze kupata matokeo mazuri.

Alisema hajaona muunganiko kwa wachezaji wake pamoja kuelewa mfumo anaouhitaji hivyo kabla ya mchezo unaofuata dhidi ya Ruvu Shooting anataka kila kitu kiwe sawa.

“Kwanza tunashukuru kwa ushindi huu wa kwanza tuliutafuta muda mrefu tukikosa, lakini niseme bado nina kazi ya ziada ya kukisuka kikosi changu kukaa sawa, sijaona kama mfumo ninaotaka wameutekeleza,” alisema Bizimungu.

Alisema ushindi huo unawapa nguvu kujipanga upya na mechi zinazofuata kuhakikisha wanashinda na kujikwamua katika nafasi ya mkiani na kupanda juu.

 “Hapa nguvu imerudi upya tunaendelea kupambana, lakini safu ya ushambuliajia nayo lazima niifanyie marekebisho kwa kuwa bado inapoteza nafasi za wazi,” alisema Kocha huyo Mnyarwanda.