Mwadui mzuka umepanda unaambiwa

Muktasari:

  • Mwadui imeanza msimu huu vibaya ikiwa imeshinda mechi mmoja ikiburuza mkia katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi tano.

Dar es Salaam. Kikosi cha Mwadui kinaendelea kujifua kikijiandaa na mchezo dhidi ya Ruvu Shooting utakaochezwa kwenye Uwanja wao wa nyumbani Mwadui Complex, kesho Ijumaa.
Wakiwa wanatoka katika mazoezi ya mwisho waliyoyafanya leo jioni, wachezaji hao walikuwa wanaonekana wana furaha na wakicheza nyimbo huku wakijirusha.
Muonekano huo unaonyesha Dhahiri wamejipanga kuhakikisha kwamba wanapata matokeo katika mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa mkali.
Kocha wa timu hiyo Ally Bizimungu, alisema wachezaji wake amewataka wawe na amani na hali hiyo inaonyesha kabisa kwamba wanatoka na ushindi katika mchezo huu.
“Kambini tupo vizuri nina amini kwamba kila kitu kitaenda sawa katika mchezo huu, kikubwa ni kumuomba Mungu na kuona mambo yanaendaje kuhakikisha tunapata matokeo,” alisema Bizimungu.