Mwadui FC yafufukia kwa Mbao

Muktasari:

Ushindi huo unaifanya Mwadui kufikisha pointi 22 sawa na Mbao lakini wakitofautiana idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.

BAADA ya kupambana muda mrefu bila mafanikio, hatimaye leo Jumamosi Mwadui FC imeamka usingizini na kuilaza Mbao FC mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa.
Mchezo huo ambao ulikuwa muhimu kwa pande zote kuhitaji ushindi ili kujiweka nafasi nzuri katika msimamo, ilishuhudiwa timu zote zikicheza kwa nidhamu na kujilinda pamoja na kushambulia.
Kipindi cha kwanza licha mashambulizi lakini umakini mdogo kwa safu ya ushambuliaji timu zote ziliwafanya kwenda mapumziko kwa nguvu sawa bila kufungana.
Mwadui walirejea kwa kasi kipindi cha pili na kufanikiwa kutangulia kupata bao lililofungwa na Raphael Aloba dakika ya 65 kwa mpira wa faulo ulioenda moja kwa moja wavuni na dakika ya 82 Wazir Junior akaisawazishia Mbao.
Hekaheka iliendelea huku kosa kosa zikijitokeza ambapo dakika nne za nyongeza, Jackson Kataga aliweza kutuma shuti kali ambalo lilimuacha kipa wa Mbao, Bruno Thomas akibaki ameshika kichwa kwa mshangao.
Matokeo hayo yaliwafanya mashabiki wa Mbao kuonekana kukata tamaa kutokana na mwenendo wa timu hiyo kwani baada ya mchezo huo wanapaswa kutoka nje kwa michezo mitano mfululizo.

Msimamo wa Ligi Kuu Bara 2019-2020
                           P       W     D     L       F     A     Pts
1. Simba                  23     19     2      2      47     11      59  
2. Azam FC                24     13      6      5      31     16    45
3. Namungo                23       13     4      6      29     21     43
4. Yanga                   21       11      7      3      25    18     40
5. Coastal Union          23       11      5      7      24     17     38
6. JKT Tanzania           24       10      8      6      23    20     38
7. Kagera Sugar           24       11     4     9      30     22     37
8. Polisi Tanzania         24       11      4      9      26     24     37
9. Biashara United    23       8      8     7      16     16     32
10.Ruvu Shooting         24       9      5      10      21     27     32
11.Tanzania Prisons   23       6     12    5      20     16     30
12.Lipuli                  23      8      5      10      30     29     29
13.Alliance FC             23       7      7      9      21     28     28
14.Ndanda                  24       6      8     10      16      19     26
15.Mtibwa Sugar       24       6      6      12     15     24    24
16.Mbeya City              24       5      9      10      17     29       24
17.Mwadui                  23       4     10      9      20       29     22
18.Mbao                    24       5     7      12     19     31     22
19.KMC                     24       5      6      13      20     30     21
20.Singida United     23       2      5     16      12      35     11

WAFUNGAJI:
13 Meddie Kagere(Simba)
10 Reliants Lusajo (Namungo)
9  Yusuf Mhilu (Kagera)
8  Paul Nonga (Lipuli)
    Daruwesh Saliboko (Lipuli)
    Obrey Chirwa (Azam)
   Peter Mapunda (Mbeya City)
7 David Molinga (Yanga)
   Ayoub Lyanga (Coastal Union)
   Bigirimana Blaise (Namungo)
   Wazir Junior (Mbao)
6 Athuman Miraji (Simba)
   Adam Adam (JKT Tanzania)
   Hassan Dilunga (Simba)
   Sixtus Sabilo (Polisi Tanzania)
   David Richard (Alliance)