Mtoto wa Masogange aibukia Bongo Muvi

Thursday December 6 2018

 

By Nasra Abdallah

Msanii wa filamu,Rammy Galis, anatarajia kucheza filamu na mtoto wa marehemu Agnes Gerald maarufu Masogange, Sania Sabri baada ya baba take kumtaka afanye hivyo.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo Alhamisi, kuhusu uzinduzi wa filamu ya 'Hukumu Yangu' ambayo aliicheza na Masogange enzi za uhai wake.
Galis amesema mbali ya baba take kutaka acheze pia mtoto mwenyewe ana kipaji na hata shule wenzake walikuwa wanalitambua hilo.
"Mtoto mwenyewe amekuwa akinisumbua kila siku kwa kuniuliza Dady tunacheza  lini filamu yetu, nilichokuwa nikimjibu ni asubiri kwanza tutoe filamu tuliyocheza na mama na ninashukuru ameniaelewa," amesema Galis.
Kuhusu uzinduzi wa filamu hiyo ya 'Huku Yangu' , amesema inatarajiwa kuzinduliwa Desemba 15 mwaka huu katika ukumbi wa City Mall.
Galis amesema katika uzinduzi huo uliopewa jina la 'usiku wa  mashuhuri' pia utakutanisha watu mbalimbali maarufu wakiwemo wacheza mpira, wanamuziki, waandaji wa kazi za muziki na filamu.
Baba wa Sania, Sabri Shabani,amesema mtoto wake amekuwa ndoto ya kuwa muigizaji tangu akiwa na miaka tisa japokuwa ameeleza atamruhusu kuingia rasmi   pale tu atakapokuwa amejitambua na kusoma kiwango cha elimu ambacho atakuwa ameridhika nacho.
Wakati upande wa filamu, amesema anashukuru kila kitu Galis amesema sawa katika suala zima la mapato yatakayopatikana.
Kwa upande wake mmoja wa wasanii walioigiza katika filamu hiyo, Hashim Kambi, amesema filamu hiyo imejaa ujumbe ambao utakuwa na faida kwa jamii kuhusiana na masuala ya utumiaji na biashara ya dawa za kulevya.
Mauzo ya filamu hayo asilimia 25 ya mauzo yake yanatarajiwa kupelekwa kwa familia ya baba wa Masogange na mtoto wake.

Advertisement