Mtibwa waipania Ligi

Muktasari:

  • Mtibwa Sugar ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara mbili ambapo ya kwanza ilikuwa ni mwaka 1999 na wakautetea tena mwaka 2000.

WAKATI timu mbalimbali zikianza mazoezi  kujiandaa na mechi zilizobakia za ligi Mtibwa Sugar wametamba kuwa hawana shaka na kikosi chao.
Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobius Kifaru anasema, wao hawana Shaka na wachezaji wao kwa kuwa wote wanajitambua na wanaelewa majukumu yao.
Anasema, hata walipokuwa majumbani kwao walikuwa wakifanya mazoezi yao kwa maelekezo ya kocha wao Mkuu Zuberi Katwila.
"Sisi tunaendesha timu yetu kisasa zaidi hatuna wasiwasi na wachezaji wetu kwani uwezo wao kila timu inaujua vilivyo,"
Mtibwa Sugar inashika nafasi ya 14  ikiwa na pointi 33 licha ya tambo za Kifaru msimu huu timu hiyo haikufanya vizuri katika mechi zilizopita kama misimu mingine.
Bosi ya Ligi kupitia kwa Mtendaji wake Mkuu Almas Kasongo alitangaza jana kuwa  ligi zitarejea kuanzia Juni 13 na Jumapili hii ratiba rasm itawekwa wazi.