Mtibwa Sugar yavuliwa ubingwa Kombe la FA

Muktasari:

Mechi ya Singida United na Coastal Union inachezwa Uwanja wa Chamazi Complex saa moja jioni. Kesho Jumapili Yanga watacheza na Namungo FC kwenye Uwanja wa Majaliwa wilayani Ruangwa Mkoa wa Lindi..

Dar es Salaam. Timu ya Mtibwa imetema rasmi ubingwa wa Kombe la FA baada ya kufungwa mikwaju ya penalti 4-3 dhidi ya KMC kwenye mchezo uliopigwa Uwanja wa Chamazi Complex.

Timu hizo zililazimika kwenda hatua ya mikwaju ya penalty baada ya kumaliza dakika 90 wakifungana bao 1-1.

Michezo mingine iliyopigwa leo, Kagera Sugar ameifunga Boma FC ya Mbeya mabao 2-1

Lipuli FC ikiizamisha Dodoma FC mabao 3 -1

Pia mechi ya Singida United na Coastal Union inachezwa Uwanja wa Chamazi Complex saa moja jioni.