Mtibwa Sugar waipa nusu Santos

Muktasari:

  • Bayser ushiriki wetu katika mashindano ya kimataifa upo palepale tayari tumeshaanza kupunguza deni tunalodaiwa na hadi ifikapo Desemba tutakuwa tumeshamalizana na Santos

KLABU ya Mtibwa Sugar imeanza kupunguza deni kwa kuwalipa kiasi cha fedha klabu ya Santos ya Afrika Kusini ambapo wanatakiwa kulipa dola 1500.
Mtibwa walitakiwa kulipa deni hilo ikiw ani faini ya kushindwa kwenda kucheza mechi ya marudiano na timu hiyo iliposhiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2002, hivyo Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kutoa adhabu hiyo.
Mkurugenzi wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser aliliambia Mwanaspoti kuwa wanatarajia kumaliza deni hilo Desemba ambapo michuano hiyo inaanza mwezi ujao, Novemba huku Mtibwa ikishiriki baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la FA.
Alisema uhakika wa kushiriki mashindano hayo upo kwasababu tayari wamekaa meza moja na Santos na wamekubaliana kulipata kiasi hicho kkwa awamu.
Bayser aliwataka mashabiki wa soka nchini kutokuwa na hofu juu yao kwani jitihada wanazofanya ni kubwa na watashiriki.
"Tumelipa nusu ya deni sitaki kukwambia ni kiasi gani kikubwa wanasoka wanatakiwa kufahamu kuwa tumeanza kulipa na tunatarajia kukamilisha deni lote hadi ifikapo Desemba tutakuwa tumekamilisha," alisema.
Bayser alisema kwasasa kikosi chao kinajiandaa na mashindano hayo chini ya kocha Zuberi Katwila huku wakiwa na imani kubwa ya kufanya vizuri.