Mtibwa Sugar inakwenda hivi Afrika

Muktasari:

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Klabu ya Simba ndiyo waliiwakilisha Tanzania msimu uliopita katika mashindano ya Kombe la Shirikisho na Yanga ilicheza Ligi ya Mabingwa Afrika.


Dar es Salaam. Kikosi cha Mtibwa Sugar kimetaja jumla ya wachezaji 26, watakaoiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Mtibwa Sugar ndiyo timu pekee kutoka Tanzania itakayocheza mashindano hayo kwa mujibu wa kanuni baada ya kuwa mabingwa wa Kombe la FA msimu uliopita.
Wachezaji hao ni Shaaban Kado, Benedictor Tinocco, Aboutwalib Mshery, Ally Shomary, Salum Kanon, Issa Rashid, Hassan Mganga, Dickson Daud, Dickson Job na Hassan Isihaka.
Wengine ni Shaaban Nditi, Henry Joseph, Saleh Khamis, Awadh Juma, Ally Makarani, Ayoub Semtawa, Salum Kihimbwa, Ismail Mhesa, Haruna Chanongo, Nassor Seif na Jaffary Kibaya.
Wapo pia, Juma Liuzio, Stamil Mbonde, Kelvin Sabato, Rifat Khamis, Cassian Ponera.
Michuano hiyo mikubwa Bara la Afrika inatarajiwa kuanza rasmi Novemba 27, lakini mpaka sasa ratiba ya CAF bado haijatoka.
Mbali na Mtibwa Sugar timu nyingine za ukanda wa Afrika Mashariki zinazoshiriki Kombe la Shirikisho ni pamoja na Zimamoto kwa Zanzibar, Uganda ni KCCA, Burundi itawakilishwa na Vital'O, kwa Kenya ni Kariobangi Sharks na Rwanda ni Mukura Victory Sports.
Wakati Simba SC yenyewe itaiwakilisha Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.