Msikie Maugo baada ya Simba kumchapa Mwarabu

Muktasari:

  • Bondia huyo mwenye tambo nyingi anapojiandaa kuzichapa ambaye pia ni mnazi mkubwa wa Simba anakwambia, kipigo cha mabao 3-0 si cha kitoto, huo ni mwanzo mzuri kwa Simba.

USHABIKI raha sana hasa timu unayoishabikia ikifanya vizuri kama ilivyofanya Simba Juzi Jumamosi pale Uwanja wa Taifa.

Ushindi wa mabao 3-0 iliyoupata Simba umemuibua bondia, Mada Maugo ambaye anakwambia hakuna kama Simba nchini hivi sasa.

“Yanga sasa kimyaa! hawana cha kuongea tena, nadhani huko waliko pamoja na kwamba hawawezi kusema hadharani, lakini watakuwa wanakubali kiwango cha Simba,” alisema Maugo.

Bondia huyo mwenye tambo nyingi anapojiandaa kuzichapa ambaye pia ni mnazi mkubwa wa Simba anakwambia, kipigo cha mabao 3-0 si cha kitoto, huo ni mwanzo mzuri kwa Simba.

“Lazima tushinde, timu haina njaa, wachezaji hawajawahi kulalamika kucheleweshewa mishahara, hatuchangishani ili timu isafiri, sasa tunashindwaje kucheza mpira mwingi kama wa Jana (Juzi),” alisema bondia huyo.

Alisema kwa namna kikosi cha Simba kilivyo, wala hawana presha kwamba wanakwenda DR Congo kuchukua pia pointi tatu na kuzidi kujikita kileleni kwenye kundi lao.

“Upande wa pili watasubiri sana kwa Simba hii, kwani sasa hivi timu hiyo ni habari nyingine katika anga za soka.”