Msigwa naye anasomeka hivi

Muktasari:

  • Msingwa aliwahi kuichezea Yanga kuanzia mwaka 2007 – 2010, timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes 2006, kusimamia na kuvumbua vipaji vya vijana wanaocheza mpira wa miguu kuanzia miaka 7 hadi 20 ndani ya mkoa wa Iringa na Tanzania kwa ujumla, kuvumbua vipaji kwa kushirikiana na TFF katika kuendeleza soka nchini.

MWANAMICHEZO na mwanachama wa klabu ya Yanga Ally Omary Msigwa ni mgombea nafasi ya ujumbe katika uchaguzi mkuu wa Yanga unaotarajiwa kufanyika Mei 5 mwaka huu.

Msigwa aliingia kwenye mchakato huo tangu unasimamiwa na Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) na sasa ameungana na wagombea wengine waliochukua fomu kupitia Yanga baada ya kufikia makubaliano ya pamoja na kushirikiana kwa pande hizo mbili, Yanga na TFF.

Katika mwendelezo wa kuandika CV za wagombea mbalimbali kwenye uchaguzi huo, Mwanaspoti inakuanikia CV ya mgombea huyo.

Msigwa ana elimu ya sekondari, pia alisomea mambo ya kompyuta pamoja na kozi ya ukocha ngazi ya awali (Intermediate Coaching Level).

Ni mfanyabiashara ambaye anamiliki Kampuni ya Alishati Investments CO. Ltd pamoja na Kituo cha kukuza vipaji cha mpira wa miguu kiitwacho Iringa Football Academy ‘IFA’, pia ni mkulima na mfugaji.

Kwenye ngazi ya uongozi, Msigwa ni kocha, Mkurugenzi Mtendaji Iringa Football Academy ‘IFA’, Mjumbe wa Chama cha Umoja wa Vituo vya Soka la Vijana Tanzania ‘TAFOCA’, Mjumbe wa Chama hicho Nyanda za Juu Kusini, Mjumbe Kituo cha Rolling Stone – Arusha, Mjumbe Kamati ya utendaji Tawi la Yanga Iringa na Nyanda za Juu Kusini, Mjumbe Kamati ya Kuvumbua vipaji mkoa wa Iringa kupitia UMITASHUMITA na UMISSETA, Mjumbe Chama cha Makocha Mkoa wa Iringa TAFCA na Mwanachama wa SPUTANZA

Msingwa aliwahi kuichezea Yanga kuanzia mwaka 2007 – 2010, timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes 2006, kusimamia na kuvumbua vipaji vya vijana wanaocheza mpira wa miguu kuanzia miaka 7 hadi 20 ndani ya mkoa wa Iringa na Tanzania kwa ujumla, kuvumbua vipaji kwa kushirikiana na TFF katika kuendeleza soka nchini.

UBINGWA AKIWA MCHEZAJI

Mwaka 2006 Mabingwa CECAFA Junior akiwa na Ngorongoro Herous mashindano yalifanyika Burundi, 2007 – 2008 Ubingwa wa Ligi Kuu Bara akiwa Yanga, 2008 – 2009 Ubingwa Yanga, mwaka 2009 Ubingwa wa Tusker Challenge Cup akiwa Yanga.

USHIRIKI MICHEZONI AKIWA MCHEZAJI

Ameshiriki Umitashumita, Umisseta, Ligi daraja la tatu na la pili (Ruaha na Magereza FC), Ligi daraja la kwanza (Lipuli FC), Ligi Kuu (Yanga), Ngorongoro Heroes, Taifa Cup (mkoa Iringa), Mgombea nafasi ya mwakilishi wa vilabu manispaa ya Iringa.