Mshiko wamzuia Nduda Msimbazi

Friday January 11 2019

 

By THOMAS NG’ITU

KIPA Said Mohammed ‘Nduda’ mbishi sana. Mabosi wake pale Msimbazi waliamua kumtoa kwa mkopo kwenda Ndanda FC, unaambiwa mpaka sasa jamaa kagoma akidai kwanza adakishwe mshiko wake.

Inaelezwa kuwa tangu Simba itangaze kumtoa kipa huyo iliyemsajili msimu uliopita kutoka Mtibwa Sugar, hajaenda Ndanda na alipoulizwa alisema, ameshindwa kujiunga na timu hiyo baada ya kutolipwa baadhi ya madai yake anayotaka kabla ya kwenda.

“Kuna pesa za usajili wangu ambazo natakiwa nimaliziwe na Simba, kiongozi wangu alisema atanipa baada ya mechi dhidi ya Nkana FC, lakini hakunipa mpaka leo, kule pia bado hawajanipa baadhi ya mahitaji ambayo yapo katika makubaliano yetu ila nikikamilishiwa nitaondoka tu,” alisema.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori, alikiri mchezaji huyo anadai na aliahidiwa kupewa pesa hizo baada ya mechi dhidi ya JS Saoura itakapochezwa.

“Sio yeye tu ambaye anadai, pesa tutatumia kwa maandalizi ya mchezo huu. Nduda anadai 5 milioni na atalipwa lakini bado amegoma kwenda Ndanda anataka kuendelea kufanya mazoezi huku mpaka alipwe pesa, kitu ambacho hakiwezekani kwa sababu hayupo katika usajili

Advertisement