Msemo wa Simba ‘kituo kinachofuata’ wamkumba Massau Bwire

Muktasari:

Aliendeleza na tambo zake  kabla ya mchezo kwamba maana halisi ya kupiga picha ya Simba, aliye ndani ya senyenge ameoanisha na kuonekana wamo ndani ya gari kutaja vituo.

KWA namna anavyojiamini msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwile unaweza ukagairi kuingiza timu uwanjani, lakini amejikuta akiwaachia Simba pointi tatu baada ya timu yake kukubali kipigio cha mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa leo Jumanne usiku.

Jana Jumatu Bwile alionekana amepiga picha akimuonyesha Simba aliyekuwa ndani ya senyenge, ametoa tafsiri yake kwamba wanacheza na timu ambayo wanaweza wakaifanya chochote.

 Awali alisema amezisikia kejeli za Simba kwamba kituo kinachofuata ni Ruvu, amekubaliana nao kwa sharti hawatapandisha mtu badala yake watashusha pointi tatu.

"Kauli yao ya kituo kinachofuata inaonyesha ni watu walio ndani ya gari, kuna mawili kushusha na kupandisha abiria kwa kuwa Ruvu haturuhusu kupandisha watu basi watashusha pointi.

"Baada ya kushusha pointi tatu tutawaacha waendelee kuokoteza okoteza dhidi ya wengine ambao watacheza bao baada ya kucheza na sisi"anasema.

Aliendeleza na tambo zake  kabla ya mchezo kwamba maana halisi ya kupiga picha ya Simba, aliye ndani ya senyenge ameoanisha na kuonekana wamo ndani ya gari kutaja vituo.

 Kama kawaida yake Bwile anayemiliki simu saba, alisema anafanya kazi kisasa na amejitambua ni mtu wa watu hivyo anapenda kupatikana muda wote.

"Nilijaribiwa kwa kuibiwa na mashabiki wa Yanga, lakini nikasamehe kwa sababu walichukua moja nikaona itamsaidia kiuchumi ila tayari nimenunua nyingine.

"Nazichaji kwa wakati ikitokea zimeita kwa pamoja napokea ya muhimu, sijawahi kuchoka kuzibeba kwani nilishakubaliana na hali hiyo,"anasema.