Msanii Danzak achomoka na Loco, awataja Diamond, Ali Kiba

Wednesday March 27 2019

 

By CHARITY JAMES

MSANII wa muziki wa muziki wa kizazi kipya nchini ambaye pia ni rubani, Ham­dan Zakwani maarufu kama ‘Danzak’ amesema anawahofia Ally Saleh 'Alikiba' na Naseb Abdul 'Diamond' katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya.

Hayo ameyasema Dar es Salaam leo alipokuwa akitambulisha nyimbo yake mpya inayokwenda kwa jina la Loco na kuweka wazi kuwa ukubwa wa majina ya nyota hao katika tasnia hiyo unampa wakati mkubwa kuhakikosha anapambana kufilia levo zao.

"Loco ni wimbo wangu unaomzungumzia mwanamke wa kiasili ambaye nampenda na kumwambia hisia zangu Lakini kwake inakuwa vigumu kuelewa nimeachia rasmi leo nipo na ndugu yangu tajiri wa mapenzi Kasimu Mganga,"alisema Danzak.

Aidha alisema kuwa japo anaishi nje lakini amekumbuka nyumbani ambapo anatarajia kuwatembelea  watoto wasiojiweza kivijini kwao Mkoani Tanga.

"Mimi ni mzaliwa wa Tanga muziki sijaanza jana wala leo nilianza zamani nikiwa Tanzania lakini nilikosa sapoti kutoka kwa wazazi na ndipo nilipoamua kurudi shule kama wazazi walivyotaka baada ya kumaliza sasa nimerudi rasmi kwenye muziki na natarajia kuwekeza huko,"alisema.

Advertisement