Msafara wa mashabiki wakwama mpakani

Muktasari:

Zambia ni miongoni mwa nchi ambazo zimekuwa na sheria ya kuzuia magari kutembea barabarani nyakati za usiku kwa hofu ya usalama.

Msafara wa mashabiki Watanzania wanaoelekea Lesotho kuishangilia timu ya taifa 'Taifa Stars' umekwama mjini Tunduma ambako kuna mpaka wa Tanzania na Zambia kutokana na kuchelewa kupata kibali cha kusafiri usiku.
Kutokana na sheria ya nchi ya Zambia inayozuia magari kutembea usiku, msafara huo umetakiwa kulala hapo mpakani kabla ya kuanza safari ya kwenda Lesotho jambo ambalo limeleta hofu ya kuchelewa kufika kwenye mji wa Lesotho ambako mechi ya Stars itachezwa.
Maofisa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wamekuwa kwenye jitihada za kuomba kibali cha kuruhusu mashabiki hao kusafiri usiku jambo ambalo limeonekana kuwa gumu kukubalika.
Hata hivyo, taratibu nyingine zote za kisheria hasa ugongaji mihuri wa hati za kusafiria kwa watu wote walio kwenye msafara huo zimekamilika na kinachongojewa na safari