Msafara mashabiki Stars wafika Mpakani

Muktasari:

Msafara huo wenye takribani watu 55, unaelekea Maseru, Lesotho kwa usafiri wa basi la timu ya taifa 'Taifa Stars'

Takribani mashabiki 55 wanaosafiri kwenda Lesotho kuishangilia timu ya Taifa 'Taifa Stars' wamewasili mjini Tunduma ambako ni mpaka wa Tanzania na Zambia.
Msafara huo umeingia Tunduma saa 8.30 mchana tayari kwa ukaguzi wa hati za kusafiria kabla ya safari ya kuelekea Lesotho.
Baada ya kukamilisha zoezi la ukaguzi, msafara huo utaelekea Zambia kabla ya baadaye kwenda Zimbabwe, Afrika Kusini na kisha Lesotho.

Zaidi ya mashabiki 50 wamesafiri kwa basi kutoka Tanzania kwenda Lesotho kuipa sapoti Stars ambao wataungana na wenzao watakaosafiri kwa usafiri wa anga na wengine ni wale waishio nchi za Afrika Kusini, Swaziland na Lesotho ambao wamejipanga kujitokeza uwanjani, Jumapili.