Mrwanda: Ulimwengu wa nini Taifa Stars?

STRAIKA wa zamani wa Simba na Yanga, Danny Mrwanda hakutaka kufumbia macho kitendo cha kocha wa Taifa Stars, Etienne Ndayiragije kumjumuisha Thomas Ulimwengu kwenye kikosi chake, wakati alikuwa hachezi.

Mrwanda alisema timu ya taifa, inatakiwa kuundwa na wachezaji wenye viwango vya juu na sio kuchukua wachezaji ili mradi wana majina makubwa, lakini muda mwingi hawakupata muda wakucheza mechi kwenye timu zao.

“Niwe mkweli na hili lazima tulisemee, Ulimwengu muda mwingi hakucheza, hivyo kocha hakuwa na sababu yakumjumuisha kwenye kikosi chake, kwani angesubiri wakati anaocheza ambao kiwango chake kinakuwa tayari kwa msaada dhidi ya taifa lake,”alisema Mrwanda

“Hiyo nafasi ya Ulimwengu kwa sasa angemuita hata, Reliants Lusajo wa KMC kwani tayari dogo ameishaonyesha ana kitu ambacho kinaweza kuwa msaada kwa timu na kwa kuwa ni mechi ya kirafiki angepata muda wakumsoma vizuri,”alisema.

Alitolea mfano wa Farid Mussa, winga wa Yanga kwamba hajaitwa kutokana na kiwango cha chini ambacho amekionyesha mpaka sasa, licha yakutoka Hispania.