Mrithi wa Masoud Djuma atua rasmi Simba

Muktasari:

  • Simba kimeweka kambi hapo kwa ajili ya mechi dhidi ya watani zao Yanga muda wowote atakuwa amesaini mkataba wa kijiunga na Simba akichukua nafasi ya aliyekowa kocha msaidizi Mrundi Masoud Djuma.

KATIKA kuhakikisha benchi la ufundi la Simba linakuwa imara
mdhamini wa Simba Bilionea Kijana Mohammed Dewji 'MO' amempa kazi ya kutafuta kocha msaidizi  Mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Crescentius Magori.
Magori katika kuhakikisha mambo yanakwenda sawa na wala hakulaza damu alikutana na kocha wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems ambaye naye aliomba kupatiwa wasifu wa makocha watano ili aweze kumchagua mmoja na kufanya nae kazi.
Aussems alipelekewa wasifu wa makocha Juma Mgunda ambaye ni kocha wa Coastal Union, Mkurygenzi wa ufundi Mtibwa Sugar Salumu Mayanga, kocha wa KMC Mtundi Ettiene Ndayiragije na kocha Lipuli Selemani Matola na Denis Kitambi ambaye alikuwa akifundisha soka nchini Bangladesh.

Mbelgiji huyo baada ya kupitia wasifu wa makocha wote alikubaliana na Kitambi ambaye mara baada ya kumpitisha aliomba mawasiliano yake na kuwasiliana nae kabla ya siku ya Jumatatu jioni kutua nchini akafanyiwa usahili ambao ulikwenda vizuri.
Kitambi ambaye amefikia katika Hoteli ya Sea Scape ambapo kikosi cha Simba kimeweka kambi hapo kwa ajili ya mechi dhidi ya watani zao Yanga muda wowote atakuwa amesaini mkataba wa kijiunga na Simba akichukua nafasi ya aliyekowa kocha msaidizi Mrundi Masoud Djuma.
Magori alisema wanaheshimu maamuzi ya kocha wao mkuu Aussems ambaye alikuwa katika utulivu na umakini wa hali ya ju ya kutafakali kocha msaidizi ambaye atakuja kufanya nae kazi kwa maelewano makubwa tangu alivyoondoka Djuma.

Anasema baada ya hapo aliomba kupewa wasifu wa makocha ambao kati ya hao alimpitisha Kitambi na kukubaliana kuwa atafaa na anaweza kufanya nae kazi ili kuhakikisha Simba inafanya vizuri msimu huu na kufikia malengo abayo imejiwekea.
"Muda wowote kuanzia sasa tutamsainisha mkataba Kitambi ambao hatuwezi kusema ni wa muda gani kwa maana kila kitu kipo ndani ya mkataba wake na tumefanya hili baada ya kupendekezwa na kupitishwa na kocha wetu," alisema.
"Mkataba upo mezani kwetu na tumesha kubaliana na kumalizana kila kitu na Kitambi bado tu kusaini na kumtangaza kuwa rasmi anataanza kazi katika kikosi chetu kama kocha msaidizi akichukua nafasi ya Djuma ambaye aliacha nafasi hiyo wazi.
"Uongozi wa Simba unaheshimu maamuzi ya Aussems na kila ambalo atakuwa anahitaji wanamtekelezea haraka wawezavyo ili kuhakikisha yale malengo ambayo hata katika mkataba wake yapo yanatimia," alisema Magori.
"Tupo katika maandalizi na mipango ya mechi na Yanga lakini hakuna mechi ambayo wachezaji wetu wanacheza bila kupata posho ila katika mechi hii na Yanga nadhani inaweza kuzidi kutokana na ukubwa wa mchezo huu, lakini timu haitakwenda kuweka kambi kokote na itabaki hapa Dar es Salaam," aliongezea Magori.
Kabla ya kuanza kazi ya kukikoa kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Simba, Kitambi alishawahi kufundisha Ndanda, Azam chini ya kocha Muingereza Stewart Hall ambaye baadae aliondoka na alikaimu nafasi ya kocha mkuu.
Timu nyingine  alizozifundisha Kitambi ni Sofapaka na AFC Leopards zote za Kenya kabla ya kwenda nchini ya Bangladesh ambapo alikuwa katika mafundisho ya ukocha ingawa pia alipata timu ya kufundisha.