Mpepo ananyoosha tu huko Zambia mjue

Monday April 15 2019

 

By Eliya Solomon

MAMBO yameendelea kumnyookea nyota wa Kitanzania, Eliuter Mpepo ambaye alikuwamo kwenye kikosi cha chama lake la Buildcon kilichoibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Lumwana Radiants.

Katika mchezo huo ambao ni wa tano kwa Mpepo akiwa na Buildcon, aliingia kipindi cha pili na kuongeza nguvu kwenye safu yao ya ushambuliaji.

Akiuzungumzia mchezo huo, Mpepo mwenye bao moja kwenye Ligi ya Zambia, alisema ulikuwa mgumu hasa kutokana na kucheza kwao ugenini ila cha kujivunia ni alama tatu walizovuna.

“Tulichodhamiria ni kwenda kucheza mchujo wa kuwania ubingwa na timu za Ligi ya Kundi A, nadhani huko nitakutana na ushindani mwingine wa timu kubwa zaidi kwa huku Zambia ambazo ni ZESCO na Nkana,” alisema Mpepo.

Advertisement