Moyes : Wasingenifukuza Kroos angekuwa Man United

Muktasari:

Moyes alisema alikutana na Kroos na kufanya naye mazungumzo ambayo yalimfanya staa huyo kuwa tayari kwenda kujiunga na Man United.

LONDON, ENGLAND . KOCHA, David Moyes amesema kitendo cha Manchester United kumfuta kazi basi kimewaponza wenyewe kupoteza nafasi ya kumnansa kiungo wa Real Madrid, Toni Kroos.

Kwenye dirisha la majira ya kiangazi mwaka 2014, Kroos aliamua kuachana na Bayern Munich na kwenda kujiunga na Real Madrid, lakini kwa mujibu wa Moyes anachodai ni kwamba Mjerumani huyo alikuwa anakwenda kutua Old Trafford. Moyes alisema alikutana na Kroos na kufanya naye mazungumzo ambayo yalimfanya staa huyo kuwa tayari kwenda kujiunga na Man United.

Moyes alisema dili hilo lilikuwa lipo hai hadi hapo Man United ilipoamua kumfuta kazi na hivyo hata Kroos akaamua kutulizana huko Santiago Bernabéu.