Mourinho kicheko, Kane atuma salamu Tottenham

Muktasari:

 Ligi Kuu England yamesogezwa mbele hadi Aprili 30 kutokana na maambukizi ya virusi vya corona wakati Ligi ya Ulaya imesitishwa hadi mwakani.

London, England. Mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs, Harry Kane amesema anatarajia kurejea uwanjani muda mfupi ujao.

Nahodha huyo wa England, alikuwa nje ya uwanja kwa upasuaji wa nyama ambao ulimuweka nje ya uwanja tangu Januari Mosi, mwaka huu.

 Ligi Kuu England yamesogezwa mbele hadi Aprili 30 kutokana na maambukizi ya virusi vya corona wakati Ligi ya Ulaya imesitishwa hadi mwakani.

“Siko mbali na kurejea uwanjani. Nadhani naweza kujiunga na timu kati ya wiki mbili au tatu zijazo,”alisema mshambuliaji huyo.

Kane amefunga mabao 17 Tottenham kabla ya kuumia katika mchezo ambao timu hiyo ilifungwa bao 1-0 dhidi ya Southampton.

Kocha Jose Mourinho tayari amempoteza mshambuliaji Son Heung-min mwenye majeraha ambaye atakuwa nje ya uwanja wiki sita hadi nane.

“Nipo katika hatua nzuri, naweza kufanya kila kitu. Nakusanya nguvu kwa ajili ya kujenga mwili kwahiyo hoja ya msingi hapa ni kwamba niko fiti,”alisema Kane.