Mourinho apewa maujanja kumtumia Paul Pogba

Muktasari:

  • Mourinho alimweka benchi Pogba kwenye mechi ya ushindi wa mabao 4-1 iliyopata Man United dhidi ya Fulham uwanjani Old Trafford juzi Jumamosi na hivyo kufufua matumaini yake katika kuifukuzia Top Four baada ya kucheza mechi kibao bila ya kupata ushindi.

MANCHESTER, ENGLAND.JOSE Mourinho amepewa darasa la namna ya kumtumia kiungo wake ghali kabisa kwenye kikosi cha Manchester United, Paul Pogba ili kuleta manufaa.

Kocha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Uholanzi, Danny Blind, ambaye ni kinara wa zamani wa Man United, amempa maujanja Mourinho jinsi ya kumtumia Pogba na kupata huduma bora kutoka kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa.

Mourinho alimweka benchi Pogba kwenye mechi ya ushindi wa mabao 4-1 iliyopata Man United dhidi ya Fulham uwanjani Old Trafford juzi Jumamosi na hivyo kufufua matumaini yake katika kuifukuzia Top Four baada ya kucheza mechi kibao bila ya kupata ushindi.

Blind alisema: “Kitu kimoja ambacho Jose anapaswa kukifanya kwa Pogba ni kumpa maelekezo kwamba awe simpo tu uwanjani.

“Pogba ni aina ya mchezaji mwenye vitu vingi sana uwanjani, anataka kufanya hadi mambo makubwa. Kwenye kiungo anataka aguse mpira mara 100,000. Anataka kuwaonyesha ubabe wapinzani wake, awaonyesha kuwa ana nguvu kabla ya kupiga mpira.

“Lakini, bahati mbaya, kwenye Ligi Kuu England wapinzani wake wote wana nguvu sawa. Hawezi kuwashinda kwenye hilo, hivyo Mourinho anapaswa kumwaambia tu, awe anapiga pasi moja kwa moja anapopata mpira, awe simpo.”