Mourinho akikubali kipigo cha Spurs nyumbani

Muktasari:

Hivyo Mourinho ilibidi amtumie Lucas Moura kama mshambuliaji wa mwisho ambaye alikuwa akisaidiwa  na Dele Alli huku  Lo Celso na Bergwijn  wakitokea pembeni walishindwa kufua dafu mbele ya mabeki wa RB Leipzig.

Tottenham Spurs wamejiweka katika wakati mgumu katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 wakiwa nyumbani dhidi ya RB Leipzig.

Kikosi hicho cha Jose Mourinho, kilijikuta kikipoteza mchezo huo wa hatua ya 16 bora dakika ya 58 baada ya kufungwa na Timo Werner kwa mkwaju wa penalti baada ya Ben Davis kumchezea vibaya, Cuneyt Cakir.

Katika mchezo huo, Spurs ilikosa huduma ya wachezaji wao muhimu katika safu yao ya ushambuliaji, Son Heung-min na Harry Kane kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Hivyo Mourinho ilibidi amtumie Lucas Moura kama mshambuliaji wa mwisho ambaye alikuwa akisaidiwa  na Dele Alli huku  Lo Celso na Bergwijn  wakitokea pembeni walishindwa kufua dafu mbele ya mabeki wa RB Leipzig.

"Tupo katika wakati mgumu" alisema kocha wa Tottenham, Jose Mourinho: "Sina hofu na aina ya matokeo tuliyopata, tunaweza kwenda huko na kushinda. Wasiwasi wangu ni kwamba hawa ni wachezaji wetu kwa mechi zijazo hata hivyo.

"Moura hakuwa lolote, Bergwijn ndio kabisa na hata Lo Celso hakuwa hatari hata kidogo hapo ndipo shida ilipo," alisema.

Wakati Tottenham wakianza vibaya nyumbani huko Italia mambo yalikuwa tofauti kwa Atalanta walitoa dozi ya mabao 4-1 dhidi ya Valencia ya Hispania.