Monaco yang’olewa Ulaya

Wednesday November 7 2018

Monaco, Ufaransa. Kocha mpya wa Monaco ya Ufaransa, Thierry Henry, ni kama ameanza kazi hiyo kwa mikosi baada ya jana timu hiyo kung’olewa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Monaco ikiwa nyumbani ilibugizwa mabao 4-0 na Club Bruges ya Ubelgiji, kipigo kilichoifanya kuburuza mkia katika kundi A ikiwa na pointi moja.

Timu hiyo imekuwa ya kwanza kutupwa nje ya kinyang’anyiro cha ubingwa huo kwani hata ikishinda mechi mbili zilizobaki itafikisha pointi saba ambazo zimeshavukwa na Borussia Dortmund ya Ujeruman I na Atletico Madrid ya Hispania.

Akizungumza baada ya kipigo hicho Henry ambaye bado hajaonja ladha ya ushindi katika mechi tano alizoiongoza timu hiyo iliyomkuza kisoka, alikiri kupitia kipindi kigumu.

Henry ambaye aliletwa ili kuokoa jahazi baada ya timu kuuanza msimu huu vibaya ameshuhudia ikifikisha michezo 15 mfululizo ya michuano mbali mbali bila kushinda.

“Nasikitika kwamba bado sijafanikiwa kuleta mabadiliko yaliyokusudiwa hapa Monaco, tu8mepoteza mchezo muhimu wa nyumbani lakini nadhani hii ni changamoto kwetu,” alisema Henry.

Alisema atazungumza na vijana wake kwani ameona makosa waliyoyafanya katika mchezo huo na kusababisha wapoteze.

&&&&          

Kocha mpya wa Monaco ya Ufaransa, Thierry Henry, ameendelea kuwa na mwanzo mbaya baada ya kupoteza mchezo wa tano tangu atwae kibarua hicho, timu hiyo ilipofungwa mabao 4-0 na Club Bruges ya Ubelgiji, katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na kung’olewa katika mbio za ubingwa huo. 

Monaco ya Henry yang’olewa Ulaya

Advertisement