Monaco, Nice zawagombanisha Henry, Vieira

Muktasari:

  • Nyota hao wa zamani wa Ufaransa wakiwa chini ya kocha Arsene Wenger walitegeneza kikosi cha Arsenal ambacho kilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu bila ya kufungwa msimu wa 2003-04

Paris, Ufaransa. Kocha wa Monaco, Thierry Henry amesema hatakuwa adui kwa muda na bosi wa Nice, Patrick Vieira wakati nyota hao wa zamani wa Arsenal na Ufaransa watakapokutana kwa mara ya kwanza wakiwa makocha.

Vieira alikuwa kocha wa Nice mwezi Juni, kabla ya Monaco kumpa jukumu Henry mwezi Oktoba.

Wawili hao watakutana leo usiku katika mchezo wa Ligue 1, baada ya mechi hiyo awali kuhairishwa kutokana na sababu za maandanamo ya watu wanaopiga serikali ya Ufaransa.

"Vieira ni rafiki yangu ni mtu ninayemkubali sana," alisema Henry.

"Siyo tu kwa uchezaji wake, lakini hata katika maisha yake, na mchezo huu hautabadilisha chochote.

"Lakini leo ni mechi kati ya Monaco dhidi ya Nice ni mchezo muhimu, kwa sababu hiyo hatutoweza kupenda."

Wawili hao walitwaa pamoja Kombe la Dunia 1998, wakiwa na Ufaransa, pia Henry na Vieira walifanikiwa kutwaa mataji pamoja wakiwa na kikosi cha Arsenal.