Molinga, Mustafa kuikosa Zesco United

Muktasari:

Mshindi wa mechi mbili baina ya Yanga na Zesco United atajihakikishia kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu

WAKATI nyota wote wa Yanga wenye leseni za Shirikisho la Soka Afrika (Caf) wakiwa tayari kwa mchezo wa kwanza wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco United kesho Jumamosi, beki Seleman Mustafa na mshambuliaji David Molinga wataukosa mchezo huo.
Molinga na Mustafa hawajapata leseni za kushiriki mashindano hayo kutoka.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari leo Ijumaa, kocha msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila alisema kikosi chote kipo kamili isipokuwa wawili hao.
"Wachezaji wengine wote wako tayari kwa mchezo isipokuwa Molinga na Mustafa ambao bado leseni zao hazijawasil,"
"Timu iko vizuri na tumejiandaa vyema kwa mchezo na tuna imani tutafanya vizuri. Kiujumla utakuwa ni mchezo wa kuvutia," alisema Mwandila