VIDEO: Mo Dewji awashukia wachezaji wavivu Simba

Muktasari:

Katika mechi tatu za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba imepata ushindi wa mechi moja dhidi ya JS Saoura ya Algeria mabao 3-0 na kupoteza mbili kwa AS Vita ya Congo 5-0 na Al Ahly ya Misri 5-0.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Klabu ya Simba, Mohammed Dewji 'Mo Dewji'  ametangaza hali ya hatari kwa wachezaji wanaocheza chini ya kiwango ndani ya kikosi cha timu hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo
Ijumaa, Mo Dewji alisema kuwa bodi ya Simba haiko tayari
kuendelea kubaki na wachezaji ambao hawajui thamani ya jezi ya
klabu hiyo.
"Tumekubaliana kwamba wale wachezaji wasio na nidhamu na
wasiojituma basi wajiandae kuondoka lakini kama wataamua
kujitolea na kuvuja jasho lao kwa ajili ya Simba tutaendelea
nao," alisema Dewji.