Mo Dewji: Simba haina mpinzani

Muktasari:

Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara, jana Jumapili walicheza mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na kushinda bao 4-1 dhidi ya watani zao Yanga. Mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

SIKU moja baada ya kuwafunga watani zao wa jadi Yanga, mwekezaji na Mwenyekiti wa Simba, Mohamed Dewji 'Mo Dewji' amewaambia mashabiki na wanachama kuwa waendelee kutamba kwani hawana mpinzani.

Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara, jana Jumapili walicheza mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na kushinda bao 4-1 dhidi ya watani zao Yanga. Mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Simba sasa atacheza fainali ya kombe hilo dhidi ya Namungo ambao walimtoa Sahare All Stars bao 1-0, fainali hiyo itachezwa Augosti 2 mwaka huu mjini Sumbawanga.

Tayari Simba ina tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Mo Dewji leo Jumatatu asubuhi ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Istagramu kuwa manena haya ambayo yameendana na wimbo ulioimbwa na msanii wa kizazi kipya, Tunda Man ambaye pia ni shabiki wa Simba.

Maneno hayo ambayo yanapatikana pia kwenye wimbo huo aliyaandika hivi; "Sina mpinzani, wewe ni mtani, mpira uwanjani, kikombe kiko nyumbaniii, wanangu wa Simba Sports tambeni, tambeni, tambeni, Simba haina mpinzani,"