Mnguto aanza kwa Coastal Union wengine mjipange

Tuesday December 4 2018

 

By Charity James

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi na Coastal Union, Steven Mnguto amesema anatarajia kuanza na timu yake kuhakikisha inabadili mfumo wa Sports Club haraka na kufuata maelekezo ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Mnguto alisema Coastal ni wahanga wa hilo hivyo anataka kuanza nao ili waweze kuwa mfano wa kuigwa na klabu nyingine.

Alisema amepewa maagizo na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia kuhakikisha analisimamia hilo na klabu zote zinafanya hivyo haraka sana.

"Suala la kubadilishwa kwa katiba ni la lazima kwa klabu zote zinazotaka kuwa wanachama wa TFF na FIFA hivyo nikiwa kama Mwenyekiti wa Bodi nitalisimamia hili kwa uharaka huku timu yangu ikiwa ni ya kwanza kuishughurikia."

"Mimi ni mhanga wa hilo kwa Coastal na siyo timu yangu tu kuna timu nyingi zinatumia Sports Club  kama wanapenga kutumia hilo hawazuiwi, lakini sasa wanapaswa kuwa na katiba mbili ambazo nyingine itaonyesha Football Club kama inavyotakiwa," alisema Mnguto.

Advertisement