Mmarekani aja kuwasha

Tuesday February 12 2019

By Imani Makongoro

MAMBO ni moto. Yule kocha wa riadha mwenye rekodi za kusisimua, Mmarekani Ron Davis anatarajiwa kuwasili nchini kesho Jumatano tayari kwa kuinoa timu ya Taifa ya Riadha.

Ron Davis kocha pekee mwenye rekodi ya kuipa nchi medali mbili za Olimpiki mwaka 1980 anatarajiwa kuingia mkataba na Shirikisho la Riadha Tanzania (RT} ya kuinoa timu ya Taifa. RT inamtarajia kocha huyo kuipa mafanikio timu ya taifa na kuweka rekodi kwenye Olimpiki ya 2020 itakayofanyika Japan.

Akizungumza na gazeti hili jana kutoka Marekani, Davis alisema atarejea nchini Februari 13.

“Nakuja kwa ajili ya kumaliza na RT,” alisema kocha huyo kwa kifupi.

Davis ni miongoni mwa makocha wenye rekodi nzuri kwenye riadha ambaye amewahi kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa lakini pia kocha binafsi wa mwanariadha, Filbert Bay

Kiocha huyo anatarajiwa kuzishuhudia mashindano mbio za taifa za kusaka nyota wa taifa wa kushiriki Mbio za Nyika za Dunia, michuano itakayofanyika Machi mwaka huu nchini Denmark.

Advertisement