Mkwabi, Try Again, Hassanol waongoza mauaji Pemba

Muktasari:

Viongozi hao wameingia Pemba pamoja na wachezaji wao watatu Haruna Niyonzima, Rashid Juma na Shiza Kichuya.

Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Swedy Mkwabi ameongoza msafara wa Simba katika fainali za Kombe la Mapinduzi.
Fainali hiyo itachezwa saa 9:30 alasiri uwanja wa Gombani kisiwani hapa.
Mkwabi ameongoza na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Salim Abdallah 'Try Again' na aliyewahi kuwa katibu mkuu, Hassan Hassanol.
Viongozi hao wameingia Pemba pamoja na wachezaji wao watatu Haruna Niyonzima, Rashid Juma na Shiza Kichuya.
Kikosi hicho kimetua uwanja wa Ndege wa Pemba kwa ndege ya kukodi kutoka Dar es Salaam.

Mjumbe mwingine wa bodi ya wakurugenzi aliyetua Pemba ni Hussen Kitta.