VIDEO: Mkongwe Yanga: Kombinesheni ya Wawa, Juuko ni ya kimataifa

Muktasari:

Juuko na Wawa wanacheza pamoja macho hiya ya kwanza baada ya Nyoni kuumia kwenye mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi.

Dar es Salaam.  Maelewano ya kimchezo yaliyoonyeshwa na mabeki wa Simba, Juuko Murshid na Pascal Wawa katika mchezo wao  wa jana Jumamosi na JS Saoula ya Algeria, yamemwibua beki wa zamani wa Yanga,  Bakari Malima 'Jembe Ulaya' na kutamka hii ndiyo yenyewe.

Malima ambaye sasa ni Kocha wa Namungo inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza amesema Juuko na Wawa wanatumia akili, nguvu na uzoefu mzuri wa mashindano hayo.

Amesema, mechi hizo za kimataifa ndiyo sawa kwao.

Amefafanua kuwa beki Erasto Nyoni ni mzuri lakini huwa anajiamini kupita kiasi mchezoni na kusababisha makosa madogomadogo yasiyo ya lazima.

Juuko na Wawa walicheza pamoja macho hiyo ya kwanza baada ya Nyoni kuumia kwenye mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi.