Mkongwe Patricia Hillary: Sitaki tena kuolewa

Muktasari:

Sikuwahi kupata changamoto katika ndoa yangu hadi mume wangu alipofariki, ila tu sijafikiria na wala sina mpango wa kuolewa kitu ambacho nimeamua tu iwe hivyo

Dar es Salaam. Mwanamuziki mkongwe wa taarab, Patricia Hillary amesema hana mpango wa kuolewa tena.

Patricia alisema kauli hiyo siyo kwamba aliwahi kukutana na changamoto katika ndoa bali ni uamuzi ambayo amejiwekea.

“Sikuwahi kupata changamoto katika ndoa yangu hadi mume wangu alipofariki, ila tu sijafikiria na wala sina mpango wa kuolewa kitu ambacho nimeamua tu iwe hivyo.

“Maana kuna baadhi ya watu wengi waliowahi kuingia kwenye ndoa hupenda kutamka hawahitaji tena ndoa kutokana na changamoto walizozipitia katika ndani ya ndoa, ila mimi hapana kwa hilo na huwezi amini kwangu changamoto za mahusiano huwa naziona tu kwenye mitandao watu wakiwa wanalalamika,” alisema Patricia.