Mkongwe Amasha atoa zawadi ya mipira Yanga -VIDEO

Muktasari:

Ahmed aliyeichezea Yanga kati ya mwaka 1980 hadi 1983, alisema kama mdau na mwanachama anawajibika kuichangia klabu hiyo.

Dar es Salaam. NYOTA wa zamana wa Yanga, Ahmed Amasha kutoka Uarabuni ameitembelea klabu hiyo leo  na kutoa michango ya vifaa mbalimbali vya michezo,  ikiwemo mipira.

Ahmed aliyeichezea Yanga kati ya mwaka 1980 hadi 1983, alisema kama mdau na mwanachama anawajibika kuichangia klabu hiyo.

"Huu ni muendelezo wa kile ambacho nimekuwa nikipenda kukifanya, nilikuwa Tanzania tangu Jumamosi ambapo niliishuhudia Yanga ikicheza na Township Rollers.

"Nimeleta kidogo nilichojaaliwa kama sehemu ya sapoti yangu kwa Yanga. Wito wangu kwa wadau wengine na wachama wa Yanga kuendelea kujitolea," alisema.

Mbali na mipira pia alitoa bips ambazo huvaliwa na wachezaji wakati wa mazoezi na koni ambazo ni kama kingo au kituo ambacho hutumika kulingana na aina ya mazoezi yanayofanyika.

Beki huyo wa kushoto aliyewahi kuichezea timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars',  anaamini Yanga inaweza kuvuka raundi hii ya awali kama watacheza kwa kujituma nchini  Botswana.