Mkenya aishtukia Simba mapema

KOCHA wa Biashara United, Mkenya Francis Baraza amesema ubora walionyesha wapinzani wao Simba na ukubwa waliokuwa nao wataingia kwa nidhamu katika mchezo wa leo usiku.

Baraza amesema ni wazi miongoni mwa timu ambayo ipo vizuri ndani ya uwanja hapa nchini Simba ni moja wapo kwa maana hiyo lazima wawape heshima katika hilo ili uwe mwanzo mzuri wa wao kuibuka na matokeo chanya.

Amesema wanapokwenda kucheza na mpinzani aina ya Simba lazima wachezaji wake wawe na nidhamu katika maeneo mawili kwanza kukaba zaidi na kutokufanya makosa ya mara kwa mara.

“Unapocheza na timu yenye wachezaji kama wa Simba ukifanya makosa matatu hayo hayo wanaweza kuyatumia na kukuadhibu kwa kufunga mabao, jambo la pili tutafanya mashambulizi ambayo nitatamani kuona wachezaji wangu wanayatumia vizuri,” amesema Baraza na kuongeza;

“Kama tukiweza kufanya hayo mambo mawili kwa uiangalifu mkubwa naimani tutaondoka na matokeo mazuri lakini kama ikiwa tofauti na hivyo hilo linaweza kubadilika. Nafahamu Simba wametenga muda wa kutosha kutufuatilia na hivyo hivyo nasi tumefanya ili kuona tunapata matokeo mazuri dhidi yao ndio maana tumepanga kutumia wachezaji wetu saba wapya wa kigeni kama watapata vibali.”

Wachezaji hao saba wapya wa kigeni ambao Baraza amepanga kuwatumia na kuwasapraizi Simba kama watapata vibali, James Ssetuba, Joseph Zziwa, Ambrose Awio wote ni raia wa Uganda, Christian Agbesi (Ghana), Abdulwahid Yusuph (Nigeria), Kilufya Jean (DR  Congo) na Timothy Balton (Kenya).

Simba itaikaribisha Biashara ikiwa na rekodi ya kushinda mechi tatu kati ya nne walizokutana kwenye Ligi Kuu Bara tangu timu hiyo ya Mkoa wa Mara ili[popanda misimu miwili iliyopita. Mchezo mmoja tu baina yao tena uliopigwa Uwanja wa Taifa, ndio ulimalizika kwa sare.