Miss Tanzania kuondoka fedha Sh10 Milioni -VIDEO

Muktasari:

Warembo 20 kutoka kanda saba watachuana Ijumaa ijayo kwenye ukumbi wa Millenium Tower Kijitonyama

Dar es Salaam. Kamati ya Miss Tanzania imesema, mrembo atakayevikwa taji la Miss Tanzania 2019 atazawadiwa Sh10 Milioni.

Warembo 20 kutoka kanda saba watachuana Ijumaa ijayo kwenye ukumbi wa Millenium Tower Kijitonyama kusaka mshindi wa msimu huu.

Mkurugenzi wa kampuni ya The Look, Basilla Mwanukuzi amesema wameamua kutoa zawadi ya fedha ili mrembo atakayeibuka mshindi aamue nini atazifanyia fedha hizo.

Basilla aliyekuwa Miss Tanzania 1998, alisema mbali na fedha hiyo, mshindi ataiwakilisha nchi kwenye mashindano ya dunia.

Alisema kamati yao imelipia Sh 20 Milioni kwa ajili ya mshiriki wa Tanzania kwenye Miss World.

"Maandalizi yamekamilika na tayari tumepata washindi  wa mataji madogo madogo ambao watatangazwa siku ya fainali pia.