Miraji wa Coastal Union asaka timu Ligi Kuu

Wednesday June 12 2019

 

By Charity James

Dar es Salaam. Beki wa Coastal Union, Miraji Adamu baada ya kumaliza mkataba wake na klabu hiyo amesema kwa sasa yupo huru kufanya mazungumzo na klabu yoyote inayoshiriki Ligi Kuu Bara.

Miraji alijiunga na Coastal Union kwa mkataba wa miezi sita akitokea African Lyon amekanusha taarifa za kuongeza mkataba na mabingwa hao wa mwaka 1988.

Miraji alisema bado hajapokea ofa yoyote na kubainisha kuwa hata timu yake ya zamani haijaonyesha nia ya kumuongeza mkataba kwani hajapokea simu kutoka kwa viongozi wakihitaji huduma yake kwa msimu ujao.

"Kazi yangu ni mpira na ndio inaendesha maisha yangu hivyo siwezi kuchagua ni timu gani naweza kucheza kikubwa maslahi ndio mwamuzi wa yote mimi nitakipiga wapi msimu uja."

"Siwezi kuweka wazi dau langu ni kiasi gani hiyo ni siri yangu baina ya viongozi wa timu wanayonitaka na mimi mwenyewe kikubwa ni makubaliano naweza nikasema nahitaji Sh40 millioni na nikajifunga kufuatwa na baadhi ya timu kwa kuhofia dau hivyo lolote linaweza kutokea mezani ," alisema Miraji.

Advertisement