Miraji kurejea kikosini Simba baada ya wiki mbili

Wednesday March 25 2020

Miraji kurejea kikosini Simba baada ya wiki mbili,Mshambuliaji wa Simba, Miraji Athuman ,

 

By Clezencia Tryphone

Dar es Salaam.Mshambuliaji wa Simba, Miraji Athuman amesema yuko fiti tayari ameanza mazoezi ya peke yake na baada ya wiki mbili atajiunga na wenzake.

Nyota huyu aliumia kifundo cha mguu akiwa katika majukumu ya timu ya taifa ya Tanzania dhidi ya Sudan amekuwa nje tangu wakati huo.

Miraji anamshukuru Mungu anaendelea vizuri na wiki mbili zijazo atajumuika pamoja na wenzake ambayo ni faraja kubwa kwake.

Kwa sasa wachezaji wa Simba wako mapumziko ya siku 30, baada ya Serikali kusimamisha shughuli za kimichezo ikiwemo Ligi Kuu Tanzania Bara.

Miraji anasema daktari aliniambia nianze mazoezi mepesi nafanya mwenyewe na najiona kabisa naendelea vizuri sana namshukuru Mungu kwa hilo.

Advertisement