Milioni 5 za Mengi zimechukuliwa ndani ya dakika 20 tu

Muktasari:

Baada ya goli hilo wachezaji wa Serengeti Boys walionekana kuamka na kufanya shambulizi la haraka kupitia kwa Kelvin John ambaye alikimbia na mpira na kupiga pasi ya mwisho kwa Edmund John aliyeweka mpira moja kwa moja wavuni.

AHADI ya Shilingi Milioni 5 kwa kila goli ambalo litafungwa na mchezaji wa Serengeti Boys, imeweza kujibu mapema baada ya mshambuliaji wa Serengeti Boys, Edmund John kufunga goli la kuchomoa dakika 20.

Nigeria walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Olatomi Olaniyani baada ya kutokea piga nikupige golini licha ya umahili wa kipa wa Serengeti, Mwinyi Yahya mpira uliingia wavuni.

Baada ya goli hilo wachezaji wa Serengeti Boys walionekana kuamka na kufanya shambulizi la haraka kupitia kwa Kelvin John ambaye alikimbia na mpira na kupiga pasi ya mwisho kwa Edmund John aliyeweka mpira moja kwa moja wavuni.

Wachezaji wa Nigeria walizidi kufunguka na walionyesha kuhitaji ushindi na walifanikiwa kupata goli la pili dakika 28 kupitia kwa Wisdom Ubani.

Umakini wao katika kutafuta magoli ulionyesha kuzaa matunda baada ya kufunga goli la tatu dakika 36, baada ya Akinkunmi Amoo kuwatoka mabeki wa Serengeti na kuweka mpira wavuni.