Milambo: Mechi za kirafiki zitatujenga zaidi

Muktasari:

Milambo aliongeza kwamba katika mazoezi yake amekuwa akizingatia kupata magoli zaidi na kujilinda ili timu yake ipate matokeo mazuri.

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya vijana 'Serengeti Boys' amesema anahitaji mechi za kirafiki zaidi ili kukipima kikosi chake kabla hawajaingia katika Mashindano ya Afcon mwezi ujao.
Akizungumza na Mwanaspoti baada ya kumalizika mazoezi, alisema kwa kukiangalia kikosi chake akiwa yupo mazoezini ameona kipo vizuri lakini kupitia mechi anaweza akajua mapungufu yake mengine.
"Tumepata mechi za kirafiki hapa nyumbani lakini bado tunahitaji kupata za kimataifa ili tuweze kuwa fiti zaidi kwa kujifunza, lakini hivi sasa tunafanyia kazi makosa ambayo yalijitokeza tulipokuwa uturuki," alisema.
Milambo aliongeza kwamba katika mazoezi yake amekuwa akizingatia kupata magoli zaidi na kujilinda ili timu yake ipate matokeo mazuri.
Katika mazoezi ya timu hiyo, Milambo alionekana kuwataka wachezaji wake kutumia spidi katika kushambulia lakini pia umakini katika kukaba.
Serengeti Boys inakabiliwa na Mashindano ya Afrika kwa Vijana chini ya umri wa miaka 17 yanayotarajia kufanyika mwezi Aprili nchini.