Mike Tyson ajibu mapigo ya Wilder

Muktasari:

Akisisitiza hilo, Wilder alidai hakuna wakati ambao yeye sio namba moja kwenye mchezo huo hivyo haungani na wengine wote wanaosema wasingeweza kumpiga Mike Tyson kama ambavyo mpinzani wake wa pambano la pili Tyson Fury alivyokubali kuwa asingeweza kumpiga.

KAULI ya bondia Deontay Wilder aliyoitoa kwamba angemtandika “vibaya mno” gwiji wa mchezo huo Mike Tyson kama angekuwa katika wakati wa enzi zake imejibiwa kishikaji na Tyson mwenyewe huko.

Akizungumza kuelekea pigano lake dhidi ya Tyson Fury litakalopigwa Jumamosi hii, Wilder hakutaka kupepesa macho kuhusu ingekuwaje endapo angekutana na mkali wa enzi hizo aliyebandikwa jina la Iron kutokana na makonde yake wakati huo na kama angeweza kupigana naye alijibu kibabe kwamba angempeleka kuzimu.

Akisisitiza hilo, Wilder alidai hakuna wakati ambao yeye sio namba moja kwenye mchezo huo hivyo haungani na wengine wote wanaosema wasingeweza kumpiga Mike Tyson kama ambavyo mpinzani wake wa pambano la pili Tyson Fury alivyokubali kuwa asingeweza kumpiga.

Tofauti kabisa na matarajio ya wengi, Mike Tyson ukipendezwa muite “Iron” ambaye alikuwa balaa wakati wake wa kupigana masumbwi alimjibu Wilder kuwa yupo sahihi kabisa kwa alichodai kutokana na ukweli kwamba hata angekuwa yeye angejibu vivyo hivyo na akashindwa kukiri kama angempiga ama la!