Mgunda aficha silaha zake kwa Sudan

Muktasari:



Ushindi dhidi ya Sudan utaifanya Kilimanjaro Stars kukata tiketi ya kucheza hatua ya nusu fainali ya mashindano ya Chalenji mwaka huu.




Kampala. Benchi la ufundi la timu ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' limegoma kutaja mbinu litakazotumia katika mchezo wake wa mwisho wa hatua ya makundi ya mashindano ya Chalenji dhidi ya Sudan kesho.
Matokeo ya ushindi katika mchezo huo yataifanya Stars ifikishe pointi sita ambazo zitaipa tiketi ya kucheza hatua ya nusu fainali ikiungana na Kenya kutokea kundi B.
Akizungumza mara baada ya mazoezi ya leo asubuhi, kocha wa Kilimanjaro Stars, Juma Mgunda alisema kuwa mchezo huo una umuhimu mkubwa kwa timu na hivyo hawako tayari kuuza mbinu kwa adui.
"Ni kweli kuna udhaifu ambao tumeuona katika mechi mbili zilizopita kama mnavyosema. Tumeufanyia kazi katika maandalizi yetu kwa mechi hiyo.
Lakini siwezi kusema hapa udhaifu wetu au tutatumia mbinu gani na badala yake tutakwenda kuonyesha uwanjani," alisema Mgunda.
Mgunda alisema anafurahi kuona wachezaji wake wote ni wazima na ana uhakika wa kumtumia yeyote katika mchezo wa kesho utakaochezwa saa 10 jioni katika Uwanja wa StarTimes, Lug