Mgombea urais Barcelona afuta usajili wa Neymar

Muktasari:

Font amepanga kuchuana na rais wa sasa wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu na alipoulizwa kama atakubaliana na bodi ya klabu hiyo kwa sasa kumrudisha Neymar kwenye kikosi chao baada ya kukuuza kwenda PSG miaka mitatu iliyopita. Lakini, Font alisema yeye si mtu atakayeamua mchezaji gani asajiliwe au nani asiosajiliwe.

MGOMBEA urais kwenye wa Barcelona, Victor Font amesema hatakuwa na mpango wowote wa kumsajili supastaa wa PSG, Neymar na kumrudisha kwenye kikosi hicho kama atashinda kiti hicho cha urais.

Font amepanga kuchuana na rais wa sasa wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu na alipoulizwa kama atakubaliana na bodi ya klabu hiyo kwa sasa kumrudisha Neymar kwenye kikosi chao baada ya kukuuza kwenda PSG miaka mitatu iliyopita. Lakini, Font alisema yeye si mtu atakayeamua mchezaji gani asajiliwe au nani asiosajiliwe.

Wakati akifuta mpango wa kumsajili Neymar, Font alisema hata Bartomeu hataweza kufanya jambo hilo kutokana na hali ya uchumi kwenye timu kwa sasa na bila ya shaka PSG itahitaji kumlipwa mkwanja mrefu. Imeelezwa PSG itahitaji kurudishiwa Euro 222 milioni zao ilizolipa kununua mkataba wa Neymer.