Messi hii sasa sifa kila mwaka bao 40

Muktasari:

Mshambuliaji huyo wa Barcelona amekuwa ni mchezaji pekee aliyeweka rekodi ya kufunga bao 40, kila mwaka kwa miaka 10 mfululizo

Barcelona, Hispania. Lionel Messi amefunga bao la 40, kila mwaka kwa miaka 10 mfululizo baada ya kuifungia Barcelona goli la kusawazisha wakitoka sare 1-1 dhidi ya Valencia Jumapili iliyopita.
Nyota huyo wa Argentina amefunga mabao 41 hadi sasa 2018, ukiwa ni mwaka 10 mfululizo anafunga zaidi ya mabao 40 kwa klabu na nchi yake.
Tayari msimu huu amefunga mabao sita katika La Liga na kuisaidia Barcelona kuepuka kipigo msimu huu.
Messi ameendelea kuthibisha ubora wake kila mwaka kuwa ni mchezaji bora.
Nyota huyo mwenye miaka 31, mwaka huu amefunga mabao 41, lakini mabao yake mengi amekuwa akifunga kuanzia Oktoba, Novemba na Desemba.
Hata hivyo, kama atafunga zaidi ndani ya 2018, itakuwa si kwa kikosi cha Argentina.
Messi hajaitwaa katika kikosi cha timu ya taifa kitakachocheza mechi za kirafiki wiki hii, baada ya kumuomba kocha Lionel Scaloni kwa anahitaji muda wa kufikiria zaidi kuhusu hatma yake ya baadaye.
Messi alianza kufunga mabao zaidi ya 40 kwa mwaka kuanzia 2009 alipofunga mabao magoli 41 wakati huo akiwa na umri wa miaka 22, na kuonyesha kuwa yeye ni mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani.
Mshambuliaji huyo wa Barcelona amekuwa akifunga zaidi ya mabao 50 kwa mwaka na 2012 alivunja rekodi baada ya kufunga mabao 91.
MABAO YA LIONEL MESSI KWA MWAKA
2009 - 41
2010 - 60
2011 - 59
2012 - 91
2013 - 45
2014 - 58
2015 - 52  
2016 - 59
2017 - 54
2018 - 41 (hadi sasa)